Rais wa Tunisia Amtimua Ofisini Waziri Mkuu Kufuatia Kuzuka kwa Maandamano

Publish date: 2024-08-17

Rais wa Tunisia, Kais Saied mnamo Jumapili, Julai 25, alitangaza kumpiga kalamu waziri mkuu Hichem Mechichi na kusitisha shughuli za bunge kufuatia kuzuka kwa maandamano nchini humo.

Maelfu ya raia wa taifa hilo wamekuwa wakiandamana katika maeneo mbalimbali nchini humo kulalamikia kile walitaja serikali inakabiliana vibaya na janga la Covid-19.

Hata hivyo Rais Kais Saied aliwahakikishia wananchi kuwa atashughulikia tatizo hilo akisaidiwa na waziri mkuu mpya akisema anataka kuleta utulivu nchini humo.

"Tumechukua hatua hizi... mpaka hali ya Tunisia irejee kuwa shwari, mpaka tuiokoe nchi," alisema Saied kama alivyonukuliwa na shirika la BBC.

Pia soma

Seneta Millicent Omanga Akanusha Madai ya Kukamatwa kwa Kuvunja Sheria za Kafyu

Tangazo la kiongozi huyo lilipokelewa shangwe na kisha baadaye Rais Saied aliungana na maelfu ya waandamamaji katika mji mkuu Tunis.

Lakini wakosoaji wake walipinga uamuzi huo wakisema hatua ya Rais Saied ni sawa na kupindua serikali.

Waandamanaji wajeruhiwa

Wakati wa maandamano hayo, waandamanaji kadhaa walikamatwa na wengine kujeruhiwa baada ya kuanza kuwarushia polisi mawe huku maafisa wa usalama wakiwatawanya kwa kurusha vitoa machozi.

Waandamanaji hao pia walivamia afisi za chama tawala cha Ennahdha, na kuharibu kompyuta, na kuteketeza afisi ndogo za makao makuu ya chama hicho huko Touzeur.

Tangu maandamano makubwa yaliyopelekea mapinduzi ya serikali mwaka 2011 ambapo serikali ya dikteta Zine El Abidine Ben Ali, iliondolewa, Tunisia bado inakumbana na changamoto za utawala ambazo zimelemaza kutolewa kwa huduma za umma.

Taifa hilo limeshindwa kubuni serikali ya kudumu huku likikeketwa na janga la Covid-19, watu 18,000 wakipoteza maisha yao kutokana na ugonjwa huo hatari.

Mnamo wiki iliyopita, Mechichi alimfukuza kazini waziri wake wa afya kwa kushindwa kudhibiti hali ya janga hilo.

Pia soma

Katibu wa COTU Francis Atwoli Asema Anashuku Ziara za DP Ruto Uganda

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ31xgJFmqZqho2LEonnTrqWiq5mWeqK506KkrpldpLOqv8inoGavka%2B2s7WMpqKurV2gwqfBwK2gmmWdlq6vsMCmmKenXp3Brrg%3D