Homa Bay: MCA Aliyedaiwa Kuwatandika Madaktari Atafutwa na Polisi
- MCA mteula Kevin Onyango anadaiwa kumshambulia Thaddeus Owiti wa hospitali ya Rachuonyo
- MCA huyo alimshambulia Owiti wakati alikuwa akifanya mkutano na madaktari wenzake
- Onyango anasemekana kuvamia hospitali ya kaunti ndogo ya Rachuonyo Kusini akiwa na watu wengine saba na kuwashambulia afisa wa afya
Maafisa wa polisi katika kaunti ya Homa Bay wameanzisha msako dhidi ya mwakilishi wadi ambaye alidaiwa kuwatandika madaktari katika hospitali ya Rachuonyo.
Habari Nyingine: Ndege ya Kijeshi Yaanguka na Kuwaka Moto Eneo la Oltinga Kaunti ya Kajiado
MCA mteule, Kevin Onyango, anasemekana kuvamia hospitali ya kaunti ndogo ya Rachuonyo kusini na kumshambulia Thaddeus Owiti wakati alikuwa kwenye mkutano na maafisa wengine wa afya.
"Niliitisha mkutano na wahudumu wa afya hospitalini ili kuweka mikakati ya jinsi watakavyosimamia chanjo dhidi ya ugonjwa wa ukambi kwa watoto wikendi hii ijayo," Owiti alisema.
Afisa wa afya alisema Onyango alikuwa katika kundi la vijana saba ambao waliingia kwa nguvu mkutanoni na kuanza mashambulizi.
Habari Nyingine: Kibwezi: Kijogoo Ajuta Kuanika Tabia ya Ufisi kwa Wakwe Zake
MCA huyo anadaiwa kumshambulia daktari huyo kwa madai kwamba kulikuwa na mpango wa kubadilisha usimamizi katika kituo hicho cha afya.
Owiti alifichua kwamba walikuwa pia wakipanga mazishi ya mmoja wa wauguzi ambaye aliaga dunai hivi karibuni huko Kaunti ya Kisii kesho wakati MCA na vijana hao walianza kuwashambulia.
Onyango na vijana hao waliripotiwa kuvamia chumba ambacho mkutano huo ulikuwa ukifanyika na kutaka usimamishwe mara moja.
Habari Nyingine: Kathiani: Lofa Mpenda Waganga Abaki Mashakani Baada ya Ndumba Kumgeuka
Hata hivyo, mjumbe huyo alipopigiwa simu alikanusha kuwa aliwashambulia madaktari hao na dadala yake akajitetea na kudai alivamia mkutano huo kwa sababu madaktari hao hawakuzingatia itifaki za COVID-19.
Katika taarifa nyingine, TUKO.co.ke iliripoti kuwa wajumbe wawili waliokabiliwa na tuhuma za kuwaibia wenzao KSh 272K walishtakiwa.
Wajumbe wa Kendu-Bay Town Morris Ogwang' na mwenzake wa Kibiri Michael Odira walidaiwa kuwavamia wenzao mjini Kendu Bay.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 073248269.
Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZoN3g5Nmn6ilkWKvosWMppqaZZGhtrqxw5qgsJldoMK4rdOapZ2hm5Z6uK3HrpuupaVixKJ5wJ%2BwmmWRqa6nwdOwmGamkWK9sLjIrKBnoKSiuQ%3D%3D