Embakasi: Barobaro Mtundu Alazimika Kukesha Kwenye Veranda

Publish date: 2024-08-25

Sinema ya bwerere ilizuka eneo la Tel Aviv, Embakasi jamaa aliyehamia kwa mpenzi wake aliyepoteza ajira kulazimika kukesha kwenye veranda usiku mrembo alipomfukuza baada ya kumzaba kofi walipokorofishana.

Penyenye zinasema kipusa alimkaribisha jamaa kwake alipopoteza kazi na kushindwa kulipa kodi na badala ya jamaa kujibidiisha aliamua kulaza damu huku mrembo akigharamikia kodi na chakula.

Habari Nyingine: Harmonize Amburuta Ex wake Kajala na Bintiye Kortini kwa Kusambaza Picha za Uchi

“Jamaa alifura kichwa kabisa na kusahau kutafuta kazi akawa anashinda akiwasiliana na vipusa mtandaoni huku akiwatumia picha za jumba walilokuwa wakiishi na hata kuahidi kuwakaribisha kwake,” mdaku aliiambia Taifa Leo.

Penyenye zinasema wakati demu alipogundua hivyo na kumuuliza jamaa, alimrukia na kumzaba kofi.

Hatua ya barobaro ilimsinya demu naye akamfunza adabu kwa kumrusha nje.

Habari Nyingine: George Floyd: Polisi Aliyeshtumiwa kwa Kuhusika na Mauaji Yake Apatikana na Hatia, Ashtakiwa

“Nimekulisha hadi ukapata nguvu ya kunichapa eeh? Sina haja nawe tena, nenda ukapewe malazi na hao viruka njia wako,” kidosho aliwaka.

Jamaa alijaribu kumtuliza kidosho lakini wapi, majirani pia walimuunga mkono dada kwa hatua aliyochukua.

Walimtaka jamaa kuondoka ili wapate usingizi huku wakimchekelea kwa kukosa aibu na kuchezea mrembo aliyekuwa amempa makao.

Habari Nyingine: Jamaa Arejea Nyumbani Baada ya Miaka 14, Akuta Familia Ilitumia KSh 40k kwa Mazishi Yake

“Vipi wewe, unadhubutu kumpiga mrembo anayekulisha na kukuvisha kama mzazi wako? Mbona hauna shukrani kwa kuwekwa mjini ukijua wazi kuwa huna kazi? Haya, kanyaga kubwa kubwa ukafunzwe na ulimwengu. Umetusinya sana kwa tabia yako mbovu,” majirani walimsuta jamaa.

Kwa sababu ilikuwa ni masaa ya kafyu, lofa hakuwa na lingine ila kukesha nje kwenye kijibaridi hadi asubuhi ilipofika akaondoka.

Semasema zinaarifu kuwa kipusa alikatiza mawasiliano na jamaa ambaye mara kwa mara aliishi kutuma jumbe akiomba msamaha.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZYZygpVmnKaakaCutLWMm5irp5KWv7B5zK2sp5ylYq6trdmipKKjkWK4trfErJ%2BaZZussq%2FFxGatnqqRo7GiesetpKU%3D