Magazeti Ijumaa Oktoba 16: Raila na Uhuru kuanzisha siasa za BBI

Publish date: 2024-07-19

Magazeti ya Ijumaa yameangazia taarifa mbali mbali zikiwemo zile za siasa za ripoti ya BBI kwani Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wanatarajiwa kuzindua BBI hivi karibuni.

Aidha kuna taarifa pia kuhusu mkutano wa baraza la mawaziri ambao uliitishwa na Rais Uhuru kuanzia Alhamisi Oktoba 15 hadi Ijumaa Oktoba 16 katika eneo la Tsavo.

1. Standard

Gazeti la Standard limeangazia taarifa kumhusu Naibu Rais William Ruto na kampeni zake kupinga ripoti ya BBI.

Kama TUKO.co.ke ilivyokuwa imeripoti, DP Ruto alianza kampeni za kupinga ripoti hiyo wakati wa ziara yake kaunti ya Nyamira katika shule ya Sironga ambapo alisema mjadala wa BBI ni kuhusu kuunda nafasi chache za uongozi.

Licha ya kuwa ripoti hiyo haijatolewa, DP alisema inazungumzia kuhusu nafasi ya Waziri Mkuu na manaibu wake wawili.

"Wale wanatuambia kuhusu mamlaka na kutengeneza nafasi yawaziri mkuu, lakini sisi tunawaambia mjadala uwe kuhusu mwananchi wa kawaida," DP alisema.

The Star

Gazeti hili lina taarifa kuwa Jaji Mkuu David Maraga amejipata pabaya na huenda akatimuliwa hivi karibuni na tume ya huduma za mahakama (JSC).

JSC itakuwa na mkutano leo ili kuafikia uamuzi wa iwapo Maraga atatimuliwa na nafasi hiyo kutangazwa kuwa wazi.

Maraga anafaa kustaafu mwezi Januari mwaka ujao lakini JSC wanataka aondoke mapema ili mrithi wake apatikane.

Daily Nation

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kukutana na DP Ruto na mawaziri ili kutafuta uungwaji mkono kwenye suala la BBI.

DP alilazimika kuahirisha ziara yake kaunti ya Murang'a ili ahudhurie kikao na Rais hii leo.

People Daily

Gazeti la PD limeangazia uteuzi wa Rais Uhuru Alhamisi ambapo aliwapa kazi waliokuwa makamishna wa IEBC.

Waliopata kazi kama mabalozi ni Consolata Nkatha, Margaret Mwachanya na Paul Kurgat ambao sasa watachapa kazi ughaibuni.

Kuna taarifa kuwa sasa wakati umefika kwa Raila na Uhuru kuanza kurindima siasa za BBI huku zikitarajiwa kuwasha moto wa kisiasa.

Taifa Leo

Taifa Leo imeangazia wale ambao wananufaika na mpasuko ndani ya chama cha Jubilee huku urafiki wa kisiasa kati ya Rais na naibu wake ukionekana kufifia.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbYJ1g5hmpJqfka%2BytbWMoqGupZGWerC306iZmmVha3qzrcilmGamkWLCqcHRrmSkrZGjx6q%2Fx5pkrKGRqK5uxsBmmZuhXp3Brrg%3D