Samburu: Fisi awajeruhi watu 3, amuua mtoto wa miaka 10

Publish date: 2024-07-04

- Watoto wawili walivamiwa na fisi wakichunga mbuzi eneo la Suguta Marmar kaunti ya Samburu

- Fisi huyo anasemekana kuwauma mikono na miguu kabla ya waokoaji kufika eneo la tukio

- Wakazi wengine wanne pia walishambuliwa na fisi huyo na kujeruhiwa vibaya, walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Samburu.

- Mvulana wa miaka wa 10 aliaga dunia huku wengine watatu wakiendelea kupokea matibabu

Familia moja kaunti ya Samburu inaomboleza kufuatia kifo cha mwana wao ambaye alivamiwa na fisi alipokuwa akichunga mbuzi.

TUKO.co.ke imefahamishwa kuwa mvulana huyo mwenye umri wa miaka 10 alikuwa na dadake wa darasa la pili wakati alivamiwa.

Habari Nyingine: Naibu Spika Bunge la Kitaifa Moses Cheboi ahusika kwenye ajali, mmoja aangamia

Habari Nyingine: Tharaka Nithi: Kidosho ajuta kukataa jamaa kisa ni 'msoto'

Naibu kamanda wa Samburu ya kati Abdikadir Malicha alithibitisha kisa hicho Jumamosi, Septemba 26 akisema fisi huyo aliuawa baadaye na wakazi wenye hamaki.

" Wakazi wanne walikimbia kuwaokoa watoto hao lakini pia walishambuliwa na fisi huyo na kuachwa na majeraha mabaya, maafisa wa polisi pia walifika eneo la tuko, wanne hao walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Samburu.

Habari Nyingine: Man City vs Leicester: Jamie Vardy awapa Foxes hat-trick na kumaliza City kwa 5-2

"Kwa bahati mbaya mtoto mmoja alifariki dunia akipokea matibabu, Watu wengine wawili walitibiwa na kisha kuruhusiwa kwenda nyumbani," Malicha alisema.

Kulingana na shahidi, mnyama huyo aliwaacha watoto hao na majeraha mabaya akisema wakazi sasa wamejawa na hofu.

Imeripotiwa kuwa msichana ambaye ni dadake marehemu yuko katika hali mahututi na bado anapokea matibabu hospitalini humo.

Habari Nyingine: Mchezaji 'msumbufu' Mario Balotelli kuaga ukapera baada ya kumposa mwanahabari

Aidha, wakazi waliwi waliokimbia katika eneo la tukio kuwaokoa watoto hao pia walivamiwa na mnyama huyo na kuacha na majeraha mabaya, wao pia walitibiwa katika hospitali hiyo na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Wakazi wa eneo hilo la Suguta Marmar wamelalama kuwa hii sio mara ya kwanza kwa fisi kuwashambulia, visa vya aina hii vimeripotiwa kwa wingi lakini serikali ya kaunti haijawajibika.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 073248269.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbX9yhJRmqpqlkqq%2FtnnFoqqiZZGsrqux0a6fomWnlsG2eZJmmKatpZZ6rsDOraZmr5FiuqqtyppkamhencGuuA%3D%3D