Rais Uhuru ampongeza Matiang'i kwa kumaliza 'simu za Kamiti'

Publish date: 2024-08-13

- Waziri Matiang'i amekuwa 'mtu wa kazi' wa Rais Uhuru huku akionekana kupewa majukumu muhimu na Rais

- Uhuru alimpa heko Alhamisi Agosti 13 kwa kuleta mabadiliko kwenye idara ya wafungwa humu nchini

- Alisema mageuzi ambayo Matiang'i ameleta yatahakikisha 'simu za kamiti' zimefungwa

Kufikia sasa ni wazi kuwa waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i ni kipenzi cha Rais Uhuru Kenyatta kwenye serikali yake.

Rais anaonekana kuzidi kuvutiwa na utendakazi wa waziri huyo na Alhamisi Agosti 13 alimpa heko kwa kazi yake kwenye Wizara ya Usalama wa Ndani.

Habari Nyingine: Saba waorodheshwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa Spika Beatrice Elachi

Akiongea Alhamisi Agosti 13 katika chuo cha mafunzo ya askari gereza Ruiru, Rais Uhuru alisema wizara hiyo imeafikia mengi chini yake Matiang'i.

"Nataka nishukuru idara hii chini ya waziri Dkt Matiang'i na katibu wake kwa kuhakikisha mnatoa nambari za usajili wa magari ambazo zina usalama wa hali ya juu," alisema Uhuru.

Alimpongeza pia Matiang'i kwa kuendesha vita dhidi ya wahalifu ambao huwaibia Wakenya kupitia sakata za mawasiliano.

Habari Nyingine: COVID-19: Afisi za NTSA kufungwa ili kunyunyiziwa dawa

Rais alisema kwa sasa kamera za CCTV pamoja na mitambo ya kuzima mawasiliano ya simu imewekwa katika jela kadhaa ili kukabili waliokuwa wakipora Wakenya kupitia njia za mawasiliano.

"Sasa hili litasaidia kumaliza kashfa maarufu ya kupokea simu kutoka Kamiti," alisema Rais.

Alisema vifaa hivyo vya teknolojia vimewekwa katika jela zote kuu humu nchini na sasa Wakenya hawatalaghaiwa tena.

Habari Nyingine: Saba waorodheshwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa Spika Beatrice Elachi

Wakenya wamekuwa wakipokea jumbe za kuwahadaa ambazo hudai kutoka katika jela la Kamiti.

Wafungwa hudaiwa ndio hutuma jumbe hizo wakitafuta Wakenya wa kuibia fedha zao kwenye simu.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 073248269.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbIB6fJRmqZqho2LCqcHRrmSapaCku6ix2Zpkppmknq6vs8hmorCZXaDCrq3LorGaZaOeurZ52ZpkpJmdnsGqesetpKU%3D