Katekista wa Kikatoliki ajitia kitanzi
- Mwili wa Davis Gisemba ulipatikana ukining'inia juu ya paa huku akiwa na kamba shingoni
- Marehemu hakuandika kijibarua chochote kuelezea kiini cha hatua yake
- Nduuguye mwenda zake alisema kakake alihudumu kama katekista kwa zaidi ya miaka 10 na wala hakuonesha dalili zozote za kutatizika kimawazo
- Mwili wa mwenda zake uanhifadhiwa kayika makafani ya hospitali ya Kisii huku uchunguzi wa kisa hicho ukiendelea
Jamaa mwenye umri wa miaka 63 na ambaye ni katekista wa kanisa la Kikatoliki kaunti ya Kisii alijitoa uhai Juni 8.
Mwili wa Davis Gisemba ulipatikana ukining'inia juu ya nyumba yake huku akiwa na kamba shingoni katika kijiji cha Nyoero, Bonyagatanyi, eneo bunge la Kitutu Chache Kusini.
Habari Nyingine: Polisi wamsaka mjakazi aliyemuibia bosi wake asiyeona KSh 46k
Kulingana na ripoti ya K24, polisi walisema hamna kijibarua chochote cha kuelezea kiini cha kujitoa kwake uhai kilichopatikana eneo ambalo mwili wa marehemu ulikuwa.
Familia yake ilisema Gisemba alikuwa na uhusiano mzuri na familia yake, na, kwa hivyo, wanashindwa kuelewa ni nini kilimchochochea hadi akaamua kujitia kitanzi.
Habari Nyingine: Jumba la wakazi laporomoka Kericho
Mwanawe marehemu, Simon Gisemba, alisema alisikia vurugu ikitokea katika chumba cha kulala cha babake na alipokimbilia kuchunguza aliona mwili wake ukining'inia kwenye paa huku ukiwa na kamba shingoni.
"Niliikata hiyo kamba kwa haraka nikiwa na matumaini kwamba alikuwa angali hai lakini katika harakati ya kumkimbiza hospitalini, nilibaini tayari alikuwa ameaga dunia," Kijana huyo alisema.
Daniel Ondieki, nduguye mkubwa marehemu alisema, David alihudumu kama katekista kwa zaidi ya miaka 10 pasi na kuonesha dalili zozote za kutatizwa kimawazo.
Habari Nyingine: Trans Nzoia: Babu wa miaka 75 auawa na walinzi kwa madai ya kuiba miwa
Akithibitisha tukio hilo, chifu wa eneo hilo, Jared Oyaro, alisema sababu ya katekista huyo kujitoa uhai haijajulikana.
"Hata hivyo, hatuwezi puuza kwamba huenda ni kutokana na matatizo ya kifamilia. Kabla ya David kujitoa uhai, alionekana akiongea na mtoto wake, ambaye alimkabidhi kiasi cha pesa kisichojulikana," Oyaro.
Mwili wa mwenda zake unahifadhiwa katika makafani ya hospitali ya Kisii huku uchunguzi wa kisa hicho ukiendelea.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdja354hJBmopqslaC2tMDAZq6aZZueuKLAzqWgpKFdlreqwMiaZKShpJa7u7WNoaumpA%3D%3D