Coronavirus: Waziri Kagwe athibitisha visa 5 zaidi nchini

Publish date: 2024-09-06

- Kati ya watano hao waliombukizwa, watatu ni Wakenya na wawili ni raia wa kigeni

- Wagonjwa watatu ni wakazi wa Nairobi na mmoja wa kaunti ya Mombasa

- Aidha, wagonjwa wanne wamethibitishwa kupona na kuachiliwa kwenda nyumbani

- Kufikia sasa, wagonjwa 12 wamepona na wengine saba kupoteza maisha yao

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ametangaza maambukizi matano mapya ya virusi vya corona na kufikisha idadi ya wagonjwa nchini hadi 184.

Visa hivyo vipya vilithibitishwa baada ya sampuli 308 kufanyiwa uchunguzi kwa saa 24 zilizopita.

Habari Nyingine: Mshukiwa wa uhalifu auawa akifyatuliana risasi na polisi

Watatu kati ya wagonjwa hao ni Wakenya huku wawili wakiwa raia wa kigeni ambao waliwasili humu nchini karibuni.

Kulingana na Kagwe, watatu kati ya waathiriwa wana historia ya kusafiri mmoja akisemekana kutokea Tanzania na wengine wawili kutoka Uingereza na Uarabuni.

Habari Nyingine: DP Ruto awataka wakenya kutilia maanani mikakati ya serikali kukabiliana na Coronavirus

Watatu kati ya wagonjwa hao ni wanaume na wawili wanawake.

Umri wao ni kati ya miaka 39 hadi 77.

Watatu kati ya wagonjwa hao ni wakazi wa Nairobi huku wawili wakitokea mji wa Mombasa.

Hata hivyo, Waziri alithibitisha wagonjwa walioambukizwa COVID-19 wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Habari Nyingine: Mgonjwa anayeshukiwa kuugua coronavirus akamatwa baada ya kuhepa hospitalini

Kufikia sasa, Kenya imerekodi wagonjwa 12 ambao wamepona huku wengine 7 wakipoteza maisha yao.

Kagwe aliwataka Wakenya kuzidi kuzingatia mikakati iliyowekwa na wizara hiyo ili kuepuka kusambaa kwa janga hilo hata zaidi.

"Tumewaona Wakenya wengi wakizingatia maagizo, kunawa mikono, kuzingatia kafyu, kuvaa vitamvua na kuepuka misongamano ya watu na tunatoa wito kwao kuendelea hivyo. Hata hivyo, kunao wachache wakaidi, natoa wito kwao kutahadhari," waziri alionya.

Alisema wahudumu wa sekta ya jua kali kama wakaidi zaidi katika kukiuka maagizo na mikakati ya serikali ambayo imewekwa kukabiliana na janga la coronavirus.

Kagwe alitoa onyo kali kwa wahudumu wa boda boda akisema watapokonywa pikipiki zao iwapo watazidi kuwa wakaidi na kupuuza maagizo ya kuepuka maambukizi.

"Tunawaomba wanaosimamia sekta za Boda Boda kuhakikisha wahudumu wanavalia vitamvua na kubeba mteja mmoja kwa wakati mmoja jinsi inavyostahili," alisema.

Aidha, Kagwe alitoa wito kwa wahudumu katika saluni na vinyozi, mama mboga na wale wa sekta ya Jua kali kuzingatia usafi wa hali ya juu kabla ya kujuta baadaye.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdjan15fZRmmqiqn6Out7XRrqpmr5GvtrO1jKSYoK%2BVYq61tMiboK2ho52ubsLIrJhmbV2vrqqwyGalnKCZo7ZvtNOmow%3D%3D