Magazeti ya Jumatatu, Machi 30: Wabunge 50 kupimwa coronavirus kwa kutangamana na mbunge mgonjwa
Huku idadi ya visa vya virusi vya corona vikiongezeka hadi 42, Magazeti ya Jumatatu, Machi 30, yanaripotoi kuhusu onyo kali kutoka kwa Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe ambaye aliwaonya wanasiasa dhidi ya kutoa habari za kupotosha kuhusu ugonjwa huo.
Magazeti haya pia yanaripoti kuhusu hali ilivyo baada ya kafyu ya kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi kuanza kutekelezwa ambapo inadaiwa watu wawili wamepoteza maisha yao baada ya kujeruhiwa na polisi.
Habari Nyingine: AS Roma yamtambua daktari Mkenya anayeongoza vita dhidi ya COVID-19 Italia
Habari Nyingine: Nairobi: Wagonjwa wa coronavirus wafikia 42
1. People Daily
Serikali imeanzisha mpango wa kulisha familia ambazo hazina uwezo wa kujilisha kutokana na hali ya uchumi iliyosababishwa na kuenea kwa virusi vya korona.
Kupitia mpango huo mpya, gatuzi na Wizara ya Kilimo zitachunguza maeneo ambayo yana uhaba wa chakula ili kiweze kununuliwa na kutolewa kwa jamii zenye shida.
Tayari kaunti 32 zimetambuliwa kama zenye uwezo wa chakula na kufikia Jumanne, Machi 31, viongozi wa kaunti wanatazamiwa kufahamisha serikali ya taifa kiwango cha chakula walichokuza katika magala ili kutolewa wakati wa shida.
Uasin Gishu, Bungoma, Kakamega, Bomet, Kisii, Kirinyaga, Kericho, Nyandarua, Embu, Nandi, Nakuru na Murang'a ni baadhi za kaunti ambazi zina chakula kwa wingi
2. Taifa Leo
Gazeti hili linaripot kuhusu habari za kupotosha ambazo zimekuwa zikisambaa katika maeneo ya Pwani ambapo baadhi ya wakazi walidai kuwa chai ya rangi ni tiba ya virusi vya korona.
Kulingana na gazeti hili, habari hizo zilitolewa na mtoto mchanga ambaye alikuwa amezaliwa.
Miongoni mwa masharti iliyotolewa kwa tiba hiyo kufanya kazi ni kuwa chai hiyo ilitakiwa kuchemshwa kupitia moto ya kuni na kuinywa kabla ya jua kuchomoza.
Hata hivyo, madaktari walikanusha madai hayo na kusisitiza kuwa njia salama pekee ya kuzuia virusi vya corona ni kwa kujiepusha na maeneo yenye watu wengi, kuosha mikono kila mara na kukaa mbali na watu.
Wakati huo huo, serikali ya Somalia imethibitisha kuwatuma madaktari 20 nchini Italia kusaidia bara hilo la Uropa kukabiliana na virusi vya corona.
Roma iliomba msaada baada ya visa vya maambukizi kuongezeka hadi 80,000 na zaidi ya vifo 10,000.
Somalia ina visa vitatau pekee vya ugonjwa huo.
3. The Star
Waziri wa Hazina ya Taifa Ukuru Yatani anatazamiwa hii leo kuwasilisha sheria spesheli ambayo Rais Uhuru Kenyatta aliagiza ili kuwalinda wananchi kutokana na hali mbaya ya uchumi iliyosababishwa na kuenea kwa virusi vya corona
Miongoni mwa mikakati ambayo Uhuru aliagiza Wizara ya Fedha kutekeleza ni 100% ya ushuru kwa watu ambao hupokea mshahara wa KSh 24,000 na kupunguzwa kwa VAT kutoka 16 hadi 14.
Bunge linatazamiwa kujadili mapendekezo yake punde baada ya Spika Justine Muturi kufahamishwa kuhusu kitakachojadiliwa na Kiongozi wa Wengi Aden Duale ama John Mbadi.
Seneti pia itarejelea vikao vyake kujadili suala kuhusiana na virusi vya corona lakini ni maseneta 15 pekee ambao watakutana wakati wa kila kikao kuzuia msongamano itakayowaweka katika hatari ya kuambukizwa virusi vya corona.
4. Daily Nation
Gazeti hili linaripoti kuwa baadhi ya wabunge 50 na wafanyakazi wa Bunge wanatazamiwa kupimwa virusi vya korona baada ya kutangamana na Mbunge wa Rabi, Kamoti Mwamkale ambaye alipatwa na virusi hivyo.
Bunge liliwasilisha majina hayo kwa wizara ya afya.
Mwamkale anashukiwa kuambukizwa virusi hivyo na Naibu Gavana wa Kilifi , Gideon Saburi wakati wa hafla ya mazishi ya Mbunge wa Msambweni, Suleiman Dori.
Mwamkale anapokea matibabu jijini Nairobi.
5. The Standard
The Standard limemtaja Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe kama mwanamume mwenye ushawishi wakati huu nchini katika vita dhidi ya virusi vya corona.
Kagwe amepongezwa kwa kutoa taarifa yake ya kila kuhusu janga la virusi hivyo.
Wakati wa hotuba zake, Kagwe amekuwa akiwahimiza Wakenya kuwa makini na ugonjwa huo kabla uangamize taifa hili.
Taarifa nyingine katika gazeti la The Standard ni kuhusu wanandoa wapya ambao walisafiri Dubai kujiburudisha na sasa wametengwa kwa sababu ya virusi vya corona.
Wawili hao walitengwa kwa lazima wiki jana katika vyumba tofauti.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaYV4f5ZmpJqfka%2BytbWMsphmoqWirrWt065kppmTnbZuf49mrpqapaO0pnmUaWSkraCeuritjJymq6eelsOqvtSsZKSvkWK4tsDAp56apZGjrm66wGakm62enLJuucaopaOvkWO1tbnL