Jombi asaka maombi kumnasua mama watoto kutoka ulevi

Publish date: 2024-09-24

Mzee kutoka eneo la Muutine, jimbo la Meru alilazimika kusaka maombi kutoka kwa pasta ili amnasue mkewe kutokana na pepo la ulevi.

Inasemekana wawili hao walikuwa wameishi katika ndoa kwa miaka kumi na walikuwa washirika wa kutegemewa sana kanisani.

Habari Nyingne: Gavana Mike Sonko atiwa mbaroni akiwa Voi

Kulingana na Taifa Leo, mzee aligundua kuwa mienendo ya mama imebadilika kwani alianza kususia ibada za kanisani.

Uchunguzi wa mzee ulibaini kwamba alikuwa akinyemelea kwa mama pima kisiri kukata kiu cha dozi.

Habari Nyingine: Picha ya msanii Weezdom akiwa kitandani na mrembo yawaudhi mashabiki

Jambo hilo lilimsikitisha sana mzee ambaye aliamua kubisha hodi kwa pasta ili amuombee mkewe abadili mienendo kwa kuwa alihisi huenda amerogwa.

Pasta alifika bomani kwa wawili hao ila hawakumkuta mama lakini baada ya muda mfupi aliwasili akiwa amelewa chakari na kupata maombi yanaendelea.

Habari Nyingine: Mwanga wa Kiswahili: Waziri wa Tanzania alitufunza lugha wakati wa uzinduzi wa BBI

Papo hapo mama alianza kuropokwa na kumkemea pasta akisema yeye hakuhitaji maombi ya mtu yeyote.

"Hakuna haja ya kunifanyia dua kwani hamna aliye msafi. Mimi nitapambana na hali yangu msiwe na wasiwasi," mama alisema.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZ4V2fphmoailkp56or%2FApJhmpZGkuqO1jKSspqaRqMKiecyapJplp5bBsMDOZqKurJ%2Bgrm7By56tomaYqbqt