Afya yako: Sababu 3 muhimu za kuacha kutumia simu gizani
Siku hizi, watu wengi hupenda kutumia simu kitandani kabla ya kulala lakini tabia hii sio nzuri kulingana na watalamu hasa ikiwa taa itakuwa imezimwa chumbani.
Pia Soma: Afya yako: Jinsi ya kukabiliana na maumivu ya kabla na wakati wa hedhi
Kuna madhara makubwa ambayo hutokana na mwangaza wa simu (smart phone) gizani, na madhara hayo huwakumba sana watu wa umri wa kuanzia miaka 30-40 ambao katika hospitali nyingi wanatafuta matibabu.
Simu inaweza kuharibu macho yako
Pia Soma: Afya yako: Jinsi ya kuendelea kuwa na afya bora wakati wa ujauzito
Katika muda mrefu ambao nimezamia kazi hii, nimegundua kuwa mionzi ya moja kwa moja kwa zaidi ya dakika 30 na zaidi ni hatari - huathiri seli za macho na hatimaye macho yanaweza kukosa uwezo wa kuona na kumfanya mtu kuwa kipofu.
Ili kuepuka upofu, ni bora tuache au tunashauriwa kuacha kutumia simu, vikatalishi na vifaa vinginevyo vyenye skrini za LED kwenye giza - bora pia kupunguza mwangaza wa vifaa hivyo ikiwa ni lazima kutumiwa.
Vile vile simu inaweza kutatiza ama kukunyima usingizi.
Pia Soma: Afya yako: Vyakula 5 vya kujiepusha navyo ikiwa wataka kupandisha hanjamu nyingi kitandani
Mwangaza wa simu hutatiza uzalishaji wa 'melatonin', homoni ambazo hudhibiti mzunguko wa mwili kulala. Sio tu kusababisha ukosefu wa usingizi na uchovu, lakini pia huweza kusababisha madhara kadhaa ya afya ukiwamo ugonjwa wa moyo, uzito mwingi, msongo wa mawazo, na wasiwasi.
Kuna hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa saratani.
Pia Soma: Afya yako: Jinsi ya kutunza mimba kwa mwanamke mjamzito
Homoni aina ya 'melatonin' hupambana na seli hatari ambazo husababiasha saratani, hivyo basi ikiwa homoni hizo hazitazalishwa kwa viwango vinavyostahili, utakuwa katika hatari ya kupata kansa na maradhi mengine ya macho.
Ikiwa umependa maelezo haya na unahisi yanaweza kumfaa rafiki yako usikose kumfahamisha naye aweze kusoma yamfae.
Makala yameandikwa na Daktari Ali Hassan, daktari binafsi, Nairobi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZ396hZhmmJ%2BxkWLGorfOZqqampGXwm5%2FjKasoaGdqnq7rYykrJqbmJZ6rMHTrqSimV2otq7BjKCgs5mennupwMyl