Serikali yafunga shule 15 kwenye msitu wa Mau huku ikiwafurusha walio ndani

Publish date: 2024-08-19

- Serikali imesema haitarudi nyuma katika kuwafurusha watu kutoka msitu wa Mau

- Takriban watu alfu 60, 000 watafurushwa baada ya kudaiwa kunyakua msitu huo

- Tayari shule 15 kwenye msitu huo zimefungwa na watoto kutakiwa kutorejea muhula wa tatu

Mkono wa serikali unazidi kuskika katika msitu wa Mau huku waliodaiwa kunyakua sehemu ya msitu huo wakifurushwa kwa fujo na vitengo vya usalama.

Tayari serikali imefunga takriban shule 15 ambazo zilikuwa ndani ya msitu huo na kusema kuwa ujenzi wake ulifanyika kinyume cha sheria.

Habari Nyingine: Pasta Ng'ang'a kunyeyekea na Habari zingine 10 zilizopepea wiki hii

Mshirikishi wa eneo la bonde la ufa George Natembeya alisema kuwa shule hizo zimekuwa zikipata ufadhili kutoka kwa shule zilizo nje ya Mau kupitia mfumo ulioitwa 'mentor school'.

“Shule hizo hazikuwa zimesajiliwa kwani hazina stakabadhi zozote kwa kuwa ziko kwenye msitu,""Haziendeshwi na tume ya kuwaajiri waalimu TSC," aliongeza

Habari Nyingine: Mkewe tajiri Tob Cohen akamatwa baada ya mumewe kutoweka

Kulingana na Natembeya, shule hizo hazina wanafunzi wanaotarajiwa kukalia mtihani wa kitaifa mwaka huu na hivyo hazitambuliki.

Baadhi ya shule hizo ni: Kirobon Centre, Senetwet Centre, Kapsilibwo Centre, Kitoben Centre, Indianit Centre, Kabarak Centre, Noosagami Centre, Chorwet Centre, Ogilge Centre, Sebetet Centre, Olabai Centre, Koitabai Centre, Chebirbelek Centre, Chebetet Centre na Lelechwet Centre.

Serikali inapania kuokoa hekta 17, 000 za msitu huo ambazo zilikuwa zimenyakuliwa na kufanywa mashamba.

Habari Nyingine: Magavana 10 taabani kwa kukosa kulipa ushuru

Zoezi hilo litawaacha watu wa familia 10, 000 kwenye hatari ya kufurushwa makao.

Aidha, kamati ya watu kumi imeundwa ili kufanikisha shughuli ya kuwatoa wote walio katika msitu huo.

Kamati hio inaongozwa na Natembeya na inakabiliwa na kibarua cha kuwatuliza wanasiasa ambao tayari wamekerwa na hatua hiyo huku wakisema watu takriban alfu 60, 000 watabaki bila makao.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZoFxgpJmqp6qmaCurbWMspifrZ6crm6%2Fx66jnmVhanqsw8SnsJ5lnai2tcGMsJhmpZGqeqnByq5koqOZrK6nwdGuqqGZXayurbXOZqWdmZ6ee6nAzKU%3D