Uhuru asema hajawahi kuzungumza na Raila kuhusu 2022

Publish date: 2024-09-30

-Rais Uhuru Kenyatta ameomba kutohusishwa na siasa za 2022

-Rais alisema kuwa anaangazia kutimiza ruwaza ya mwaka wa 2030

-Alisema kuwa hajawahi kuzungumza na Raila Odinga kuhusu siasa za urithi wa wadhifa wa urais

Alidai kuwa alimpata mshirika (Raila) wa kumsaidia kutimiza malengo yake ya miradi ya maendeleo

Rais Uhuru Kenyatta amepuuzilia mbali siasa za urithi wa uongozi wa mwaka wa 2022 na kusema kuwa hana haja na siasa hizo.

Rais Kenyatta alisema kuwa anaangazia kutimia ruwaza ya mwaka wa 2030.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Rais alisema kuwa hajawahi kuzungumza na kinara wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga kuhusu siasa za 2022.

Habari Nyingine: Video: Wakenya wampigia saluti binti Mkorino aliyesakata densi katika harusi yake

Habari Nyingine: Seneta Millicent Omanga afichua jinsi Ruto alivyobadilisha maisha yake

Uhuru aliyasema hayo kwenye mazungumzo na wanahabari baada ya kulihutubia taifa Ijumaa, Desemba 28 jijini Mombasa.

“Hatujawahi kuzungumza na Raila kuhusu 2022 hata siku moja. Tunazungumzia kuhusu mambo tunayoweza kurekebisha na tunayarekebisha kwa ajili ya vizazi vijavyo,” Uhuru alisema.

Habari Nyingine: Matokeo ya wanafunzi 7 wa Ambira Boys waliomtusi Matiang’i, Amina

Rais alisema atashikilia mjadala wa maendeleo kwenye mazungumzo yake na Raila na watu wengine wanaoangazia jinsi Wakenya wanavyoweza kuleta maendeleo nchini kupitia kwa juhudi zao.

“Hatujawahi kuzungumza na Raila kuhusu siasa za 2022 na tumeelewana, hivyo hatuwezi kukubali siasa ambazo tumekuwa tukifanya ziendelee. Kwa nini watu wanaibua maswala kuhusu uchaguzi wakati tumemaliza uchaguzi hivi majuzi?” Uhuru aliuliza.

Habari Nyingine: Jamaa amfurusha mkewe siku 2 baada ya harusi, adai mtu aliifungua 'sava'

Rais alifichua kuwa aliwaagiza viongozi wote kukoma kuendeleza siasa za 2022 na kuangazia miradi ya maendeleo ambayo serikali ilistahili kutimiza.

“Tuangazie ajenda ya maendeleo na kuwafikia watu wote wenye misimamo tofauti ya kisiasa.

“Usiniulize kitu chochote kuhusu 2022. Acha wale wanaotaka kuyazungumzia wafanye hivyo, sio mimi. Ninaangazia ruwaza ya mwaka wa 2030,” Uhuru aliongeza.

Habari Nyingine: Mbunge wa Wajir Fatuma Gedi azungumza kufuatia video ya mahaba iliyosambaa mitandaoni

Rais Kenyatta aliashiria kuwa ataunga mkono kura ya maoni akidai kuwa lazima mifumo yote iwe inavifaa vizazi vijavyo.

“Hutaki kuwa kwenye ajenda inayosema Wakenya wazungumze na wenzao na kutafuta kujua kwa nini tuuunapigana kila baada ya miaka mitano au tutakavyohakikisha ufisadi umekabiliwa?” Rais Kenyatta aliuliza.

Read ENGLISH VERSION

Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News

Je, Krismasi ina thamani ya kusherehekewa? | TUKO TV

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiboF5hY9mrKGtoqp6or%2FEpphmoJGfrritx6JkpK2qqruowcyzmGamkWK%2ForXLmmSkrZiqwLZ5kWlpa2aYqbqt