Aibu ya kumalizia mwaka: Pasta afumaniwa kanisani akioa mke mwingine

Publish date: 2024-07-12

Mchungaji wa Kanisa la Gospel Revival Assemblies of God lililopo Mlandizi, Tanzania, Julius Andrew, amekumbwa na aibu nzito baada ya kufanya jaribio la kumtosa mkewe, Maria Stoni na kwenda kuoa mke mwingine kwa siri.

Lakini wakati mchungaji huyo akiwa katika jaribio hilo, mkewe alipata taarifa na kuvamia kwenye kanisa alilotaka kufungia ndoa hiyo.

Habari Nyingine: Picha 5 za bintiye hayati Lucky Dube ambaye pia ni mwimbaji mahiri

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Dennis Oliech aonekana akijivinjari Maasai Mara na kipusa, atumia KSh 160k kwa siku

Shughuli ya ndoa hiyo iliyotibuliwa na Maria, ilikuwa ifungwe katika Kanisa la Gospel Revival Assemblies of God, Mbagala Kuu – Tawi la Vianzi, Vikindu, wilayani Mkuranga, mkoani Pwani mnamo Alhamisi, Disemba 6. Hata hivyo, awali ratiba ilionyesha kuwa, ndoa hiyo ilikuwa ifungwe katika kanisa hilo, tawi lake la Mbagala Kuu, lakini baadaye mchungaji akaamua kubadili kanisa.

Hatua hii ilichukuliwa ili mchungaji na mke wake huyo wa pili wavishane pete bila ya usumbufu wa mke wa kwanza Maria ambaye tayari alikuwa amepata fununu.

Habari Nyingine: Binti mrembo ashangaza wengi baada ya kutangaza anaishi na virusi vya HIV

Majira ya 5 pm, maharusi hawakuwa wamefika na kisha alipofika, Andrew alidai alikuwa amepotea njia kwa kuwa kila mtu alikuwa amechukua njia yake.

Mara waipotaka kuvishana pete, Maria alimwendea mchungaji aliyekuwa akiongoza shughuli na kumjulisha kuwa, mtu aliyekuwa akifanya ndoa ni mume wake halali waliyefunga naye ndoa.

Nzule alimtaka athibitishe naalikubali ingawa alimtaka aendelee kukaa kimya kwanza.

Habari Nyingine: Aliyekuwa mtangazaji wa KTN azingua wafuasi mtandaoni akiwa nusu uchi

Wakati ulipofika rasmi wa maharusi kuvishana pete, mchungaji aliuliza ikiwa kuna pingamizi na ndipo Maria aliposimama na kutoa vyeti vya kuthibitisha ndoa.

Watu waliokuwa wamefika kushuhudia ndoa hiyo walibaki vinywa wazi. Baadhi walikuwa wachungaji na familia na marafiki na Nzule akaamua kufuta harusi hiyo ili uchunguzi kufanywa.

Hata hivyo, wakati akihotubia umma, Maria alisema hawezi kumlazimisha baba ya watoto wake wawili kukaa katika ndoa yao ikiwa amechoka.

Habari Nyingine: Vyakula 3 kutoka Mombasa vinavyodaiwa kumfanya mtu 'simba' kitandani

“Lakini kama mume wangu hanitaki tena basi tufanye mgawanyo wa mali tulizochuma pamoja. Tuna kiwanja kilichopo Mbande, pikipiki aina ya Boxer, friji, kitanda, godoro, vyombo vya ndani na pesa ya kuanzia maisha. Yakifanyika hayo, ndipo aendelee na mambo yake,” Maria alisema kwa sauti ya huzuni.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Askofu Mzule alisema ndoa ya kikristo ni ya milele na haiwezi kuvunjwa na mahakama, ingawa wawili hao wanaweza kutengana kwa sababu za kiusalama lakini ndoa yao itatenganishwa na kifo pekee.

Habari Nyingine: Dereva wa tuktuk anaswa kwenye video akiwatwanga polisi trafiki

“Hakuna ndoa ya wake wengi kwa sisi Wakristo… na ikishafungwa, imefungwa hakuna kuachana hadi kifo. Wanaweza kutengana kwa sababu mbalimbali ikiwemo za kiusalama lakini siyo kuachana. Ni kifo pekee kinaweza kutengua ndoa ya Kikristo,” alisema.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiboB1fpVmmKKapWLGonnKrqSapJmvtqJ5zLCYpJldpa60wMBmmJ%2BtnZa7qsPAZqKappmorq%2B1jJqioqeRYrqssYymrqKml567pnrHraSl