Seneta wa Meru Mithika Linturi aonywa dhidi ya kuwasiliana na mkewe baada ya kumtishia maisha

Publish date: 2024-09-29

-Seneta huyo ataruhusiwa kuwasiliana na mkewe panapo amri kutoka mahakamani

- Mkewe alipatiwa baadhi ya makazi ya seneta huyo na kumtaka asikaribie mahali popote anakokwenda

- Hii ni baada ya mkewe Mithika kumshtaki katika makao makuu ya upelelezi, DCI kwa madai kwamba alimtishia maisha

Mkewe seneta wa Meru Mithika Linturi amepata afueni baada ya mahakama kutoa amri kadhaa kufuatia vitisho vya seneta huyo vya kutaka kumuua.

Habari Nyingine: Hawa ndio wanaume 8 wanaovutia zaidi duniani?

Linturi sasa ametahadharishwa na korti dhidi ya kumtishia maisha mkewe, watoto wao watano au mtu yeyote ambaye ni jamaa wake.

Kulingana na amri hiyo ya korti, Maryanne Keitanny pia aligawiwa baadhi ya makazi ya seneta huyo ambapo atakua akiishi na watoto wao sita.

Habari Nyingine: Afueni baada ya utafiti kupata dawa ya kutibu HIV/AID

"Seneta ameonywa dhidi ya kumtishia maisha mkewe, wala watoto wake au mtu yeyote wa familia yake," Hakimu wa mahakama kuu ya Milimani alisema

Linturi pia alitakiwa kumruhusu mkewe kuingia nyumbani kwake akiwa chini ya ulinzi mkali ili kumwezesha achukue bidhaa zake.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Vyakula 3 kutoka Mombasa vinavyodaiwa kumfanya mtu 'simba' kitandani

Mahakama pia ilimtahadharisha Linturi dhidi ya kukaribia makazi au mahali popote anakokwenda mkewe.

Aidha, Linturi hataruhusiwa kumpigia mkewe simu wala kuwasiliana naye kwa njia yoyote ile pasipo na amri kutoka kortini.

Habari Nyingine: Kalonzo apata kazi siku chache baada ya kuomba kumsaidia kazi Uhuru

Seneta huyo ambaye anamiliki bastola kihalali, anasemeka kumtisha mkewe maisha kwa kutaka kupiga risasi baada ya ugomvi wa kinyumbani kuzuka katika yao.

Read: ENGLISH VERSION

Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdibn53fZFmqp6mlamubsPAZqSeqqViuqrAx6KimmWcnru1wdGiZJqnnq7EonnDoaCdoV2urm631LCYrKGcnq6vrYynmGalm5rEpnnBmpidmV2urm631KaroquYnq5uucCiqqGZXp3Brrg%3D