Afisa trafiki wa kike atekwa nyara, dereva aliyevunja sheria za Michuki adaiwa kuhusika

Publish date: 2024-09-27

- Afisa huyo alikuwa amelinasa gari hilo kwa kuwa halikufaa kuwa barabarani

- Inadaiwa afisa trafiki huyo alimshauri dereva kulipeleka gari kituo cha polisi lakini alifyatuka na kuelekea barabara ya Butere na kisha kutoweka naye

- Washukiwa wawili wametiwa mbaroni wakisubiri kuwasilishwa kortini ingawa dereva wa gari hilo

Polisi mjini Mumias, Kaunti ya Kakamega wanamsaka dereva wa matatu aliyemteka nyara afisa wa polisi trafiki wa kike na kumuumiza muda mfupi baada ya kukamatwa.

TUKO.co.ke imepata habari muhimu kwamba, kisa hicho kilitokea Jumanne, Novemba 13, kwenye barabara kuu ya Mumias - Bungoma.

Habari Nyingine: Picha ya sosholaiti Mtanzania akipapasa sehemu nyeti ya mwanaume yazua hisia mseto

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Afisa huyo wa polisi baadaye alipatikana na kulazwa katika Hospitali ya St. Mary's Mumias kisha akaruhusiwa kwenda nyumbani. alikuwa na majeraha ya kifua na shingoni.

Akithibitisha kisa hicho, Afisa Mkuu wa Polisi (OCPD) Mumias, Peter Katam alisema afisa wake alikuwa amelikamata gari lililokuwa na makosa.

Habari Nyingine: Bosi wa benki maarufu aanikwa kwa kumpokonya gavana mke

Kulingana naye, afisa wake alitaka gari kupelekwa kituo cha polisi lakini dereva alifyatuka na kuelekea barabara ya Butere.

"Maafisa wengine walifahamishwa kuhusu kisa hicho na kwa msaada wa bodaboda, walilifuata gari hilo na kulipata Shitswitswi ila dereva alifanikiwa kutoroka," Katam alisema.

Habari Nyingine: Vyakula 3 kutoka Mombasa vinavyodaiwa kumfanya mtu 'simba' kitandani

Washukiwa wawili wametiwa mbaroni wakisubiri kuwasilishwa kortini Jumatano, Novemba 14 baada ya uchunguzi kukamilika.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdibn52f5RmmJ%2Bho5Z6tb7An6CkoV2srm63yKScZpmkmri4rYynsJqqkWKxpr7Er5hmmZyexqbC1KehmmWjnbKztcBmsZplnZ6wqcHKomSanJGexKJ5yq6frquZoK5vtNOmow%3D%3D