TSC yawafuta kazi walimu 71 wa kiume ambao wamekuwa wakiwanyemelea wanafunzi wa kike
-Serikali imetishia kuwakamata walimu wa kiume ambao wako na mwenendo wa kushiriki ngono na wanafunzi hasa wa shule za msingi na za sekondari
- Zaidi ya wanafunzi 20 waliripotiwa kujifungua wakati mitihani ya kitaifa ya KCPE ilipoanza
- Hata hivyo serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi anapata nafasi ya kujiunga na shule za upili bila pingamizi lolote
Serikali imeahidi kuwakamata na kuwashtaki walimu watakaopatikana wakishiriki ngono na wanafunzi wa kike wenye umri mdogo.
Habari Nyingine : Afisa wa trafiki acheza densi barabarani, asahau habari ya hongo (video)
Habari Nyingine : 80% ya mutura zinazouzwa Nairobi zina uchafu unaosababisha magonjwa - utafiti
Hii ni kufuatia idadi kubwa ya wanafunzi wa kike kuripotiwa kupachikwa mimba na kujifungua wakati mitahani ya kitaifa inapoendelea.
TUKO.co.ke iliweza kubaini kuwa tume ya kuajiri walimu, TSC imewafuta kazi walimu 71 ambao walipatikana wakiwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wenye umri mdogo.
Akizungumza na vyombo vya habari Alhamisi Novemba 1, katibu mkuu wa Elimu Belio Kipsang' alisema serikali itafukua hadi vijijini ili kuwatafuta walimu wenye mwenendo huo na watachukuliwa hatua kali ya kisheria endapo watapatikana.
Habari Nyingine : Mtoto wa nyoka ni nyoka; bintiye Akothee ajianika nusu uchi
" Hebu na tuwapatie watoto wetu fursa ya kutimiza ndoto zao, wale wanaopitia mlango wa nyuba kuharibu maisha ya wanafunzi hasa wa kike na kukwepa mkono wa sheria, nawahakikishia kwamba tutakabiliana nao vilivyo endapo tutawakamata,"Kipsang' alisema.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine : Kutana na binti mrembo Mkorino anayewakosesha wanaume usingizi
Aidha, serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi anapata nafasi ya kujiunga na shule ya upili bila kuzingatia matokeo ya KCPE.
Read: ENGLISH VERSION
Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke ,kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News
Tazama habari zaidi kutoka TUKO TV
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdibn13hZhmq6ybXa6uuK3FrquaZZuWx6p51pqjoqWlYoRyedaaZKShpaKybq3Mm5ioZaeWuqa31LCYZq%2BRoLa4rc2ynKadnJqubsPAp5ifrZ6vtm7DwGaioqOVY7W1ucs%3D