Mbunge Naisula Lesuuda kufunga ndoa mwaka 1 baada ya kudaiwa kumchumbia Kipchumba Murkomen

Publish date: 2024-09-17

-Harusi hiyo itashuhudiwa na wageni waalikwa, marafiki na wanafamilia watakaoalikwa pekee

-Wawili hao wanafunga ndoa miezi tisa baada ya mpenziwe mbunge huyo kumpendekezea posa

Ni rasmi kuwa mbunge wa Samburu Magharibi Naisula Lesuuda atafunga ndoa na mpenziwe Jumamosi, Novemba 17, 2018.

TUKO.co.ke ina habari kuwa Naisula na mpenziwe, Robert Kiplagat, wameratibiwa kula kiapo cha ndoa katika harusi ya kihfahari eneo la Lesirai karibu ya mji wa Suguta, kaunti ya Samburu.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Pasta mrembo zaidi Kenya ajishaua kwa gari lake la mamilioni ya pesa

Habari Nyingine: Picha zinazoonyesha Jacque Maribe anajuta kuchumbiwa na Jowie

Harusi hiyo itakuwa ya wagenii waalikwa pekee watakaojumuisha marafiki na wanafamilia wa wapenzi hao.

TUKO.co.ke ina habari kuwa mbunge huyo na mpenziwe watafanya harusi katika sehemu ambapo wageni wao watapata huduma za malavi kwa ada tofauti.

Habari Nyingine: Kutana na afisa wa polisi wa Taveta anayewakosesha usingizi 'team mafisi' kwa urembo

Harusi ya Naisula na Kiplagat imejiri miezi tisa baada ya fununu kuibuka kuwa mbunge huyo mrembo kukubali pete ya posa kutoka kwa mpenziwe.

Posa yao ilijiri wakati kulikuwepo na fununu kuwa Naisula alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen.

Habari Nyingine: Picha za mazishi ya Sharon Otieno nyumbani kwa babu yake Homa Bay

Kulingana na ripoti za hapo awali za TUKO.co.ke, habari ya uchumba wa wapenzi hao zilisambaa Machi 2017 baada ya jumbe za mahaba kati yao kusambazwa mtandaoni.

Kwenye baadhi ya jumbe hizo, Murkomen alikiri penzi lake kwa binti huyo na kugharamia ziara za kimataifa wakiwa pamoja wakati ambapo seneta huyo maalum wa zamani alipokuwa akimchumbia mpenziwe ambaye alikuwa mtaalamu wa maswala ya habari na teknolojia na jina lake kubanwa.

Read ENGLISH VERSION

Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News

Bibi Cecilia awashauri mabinti kukoma kuwachumbia masponsa | TUKO TV

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibYZ1gpFmpJutnpyybrrAoqqupJFiuaa%2F1K6bmmWbqrO2usaaZKecn5Z6rsPApJhmaV2XrqKwwGawmmWbqrGitdaaZKStnZi1trnBophmo5mlsKnBzJuYZqWlp7iwucSnZaGsnaE%3D