Polisi wa kupambana na ugaidi wawakamata washukiwa Nanyuki kabla ya ziara ya Prince William Septemba

Publish date: 2024-08-23

- Polisi wa kupambana na ugaidi waliwakamata waumini 40 katika msikiti eneo la Nanyuki

- Waumini hao 40, akiwemo Imam waliaminika kuingizwa katika imani yenye itikadi kali

- Miongoni mwao walikuwa watoto 29 kutoka kaunti ya Laikipia ambao baadaye waliachiliwa kwa wazazi wao

- Waliosalia wanaoaminika kuwa washiriki wa al-Shabaab walikabidhiwa maafisa wa kupigana na ugaidi

- Prince William anatarajiwa kuzuru Nanyuki mnamo Jumapili, Septemba 30

Polisi wa kupiga vita ugaidi waliotumwa Nanyuki kuendesha shughuli ya msako dhidi ya washukiwa wa ugaidi kabla ya ziara ya Prince William wa Uingereza wamewakamata watu kadha miongoni mwao akiwa Imam.

Kisa hicho kilichotendeka katika mitaa iliyo karibu na British Army Training Unit Kenya (BATUK) Nanyuki, kaunti ya Laikipia ambapo vikosi vya Uingereza hufanya mazoezi pamoja na wenzao Wakenya.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Imam alikamatwa pamoja na 39 wengine baada ya polisi kuvamia msikiti wa Kabiru eneo la Nanyuki linaloaminika kutumika kuafunza itikadi kali vijana kutoka nje ya kaunti ya Laikipia kwa mujibu wa Daily Nation.

Habari Nyingine: 'Obado in, KDF out': picha ya mandazi mapya sokoni yasisimua Wakenya

Habari Nyingine: Mama avua nguo nje ya ofisi ya Uhuru kulalamikia 8% VAT (picha)

Miongoni mwa waliokamatwa ni watoto 29 chini ya umri wa miaka 18 ambao polisi wanaamini waliingizwa katika imani yenye itikadi kali na ambao baadaye waliachiliwa kwa wazazi wao baada ya kuhojiwa.

Waliosalia,11, wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na al-Shabaab, walikabidhiwa kwa afisi za eneo hilo la Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi (ATPU) katika kaunti jirani ya Isiolo.

Habari Nyingine: Ujumbe mtamu wa Jacque Maribe kwa mpenziwe kabla ya shutuma za mauaji kumwandama

Bosi wa Laikipia Mashariki, Mutoro Kizito, aliyeongoza msako huo msikitini alihoji waliokamatwa walikuwa washiriki wa al-Shabaab waliofikiria maafisa wa usalama walikuwa tu wakijishughulisha na wezi wa mifugo.

“Lilikuwa lengo gani la kupiga kambi hapa kwa nia ya kugeuza watu kuwa Waislamu na kufunza watoto Madrassa wakati kuna misikiti katika kaunti wanakotoka washukiwa?” alihoji.

Habari Nyingine: Makachero wanaochunguza mauaji ya Monica Kimani wakagua gari la Jacque Maribe (picha)

Prince Williams anatazamiwa kuzuru Nanyuki mnamo Jumapili, Septemba 30, kwa mara ya kwanza kama msimamizi wa Royal African Society (RAS) na pia kama sehemu ya shughuli zake za umma na kibinafsi Afrika.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibYRzgpJmp6ikmai2bsPAZqKuqJGir6K6wGalmmWlnK6qsMhmrpqvkaCurq3TmmSwmaOdwqy11ppkp5mersKstYykmJukkWLGonnZopirmV2urm680aKlnJ1drLatuMiapGarlaXBprnBmmRsaF6dwa64