Mama mkwe amtwanga na kumfurusha bintiye kwa kumuaibisha

Publish date: 2024-09-22

- Mama huyo alikasirika kugundua kuwa mkaza mwana wake alikuwa akibugia pombe, tabia ambayo si kawaida katika mtaa huo

- Aliamua kumfunza adabu kwa kumpiga akidai kuwa alikuwa akiwatia aibu

Habari Nyingine : Gavana Joho ammezea mate kipusa wa Safaricom hadharani na kuwasisimua wengi

Ilikuwa sinema ya bure katika eneo la Mugoiri, Murang’a huku mama mkwe akimtandika hadharani mkaza mwana wake baada ya kumpata akiwa mlevi kupindukia.

Kulingana na kisa hicho kilichochapishwa katika gazeti la Taifa leo, binti huyo alikuwa amedumu kwa ndoa kwa muda wa miaka mitatu.

Habari Nyingine : Jamaa amuaibisha mpenziwe kwa chupi zake chafu mtandaoni

Inadaiwa kuwa kabla kuolewa, mwanadada huyo alikuwa na tabia nzuri na alikuwa akipigiwa mfano katika mtaa mzima huku kila kijana akishauriwa kumuiga.

Cha kushangaza ni kuwa baada ya kuolewa, tabia zake zilianza kubadilika huku akianza kuwa mraibu wa pombe.

Habari Nyingine : Gavana wa Nandi amulikwa baada ya kutuma ujumbe wa kimapenzi kwa WhatsApp kimakosa

Siku ya tukio, mwanadada huyo alihudhuria mkutano ya chama ambako walipewa mvinyo. Mwanadada huyo alibugia pombe kiasi cha kujikokota akitembea.

Akiwa njiani kurudi nyumbani, alikutana na mama mkwe aliyeshangaa kumuona katika hali hiyo.

Habari Nyingine : Doreen Moraa, msichana mwenye umri wa miaka 25, hafichi hali yake ya HIV na ni mrembo ajabu

''Oh no! yani unataka kumaanisha kuwa wewe ni mlevi ilhali wewe ni mke wa mwanangu? Kamwe siwezi kukubali tabia hii hapa na lazima nikuonyeshe mimi ni nani,’’ mama mkwe alimfokea kwa hasira.

Moja kwa moja alianza kumshambulia kwa makofi bila huruma akiapa kumfunza adabu.

Habari Nyingine : Picha za kuvutia za binti yake Auma Obama, Akinyi

Mrembo huyo pia akiwa katika hali hiyo ya ulevi, alimvamia huku vita vikipamba moto.

Majirani walivutiwa na kelele zao na upesi wakaja kuwatenganisha.

Mwanadada huyo aliondoka hapo akilia na kuenda hadi kwa wazazi wake. Haikubainika kama alirudi tena kwa mumewe.

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibX15gZZmpJqlkWK6rMPEZpimrKeWu6itjKeYZqOlorO2vtSsn5plkp67tbXYnmSkr5FiuLa51Jqgm6Gjna5vtNOmow%3D%3D