Waititu amfuta kazi waziri anayependa kutumia mitandao ya kijamii
-Gavana Waititu amemsimamisha kazi afisa mmoja mkuu mtendaji katika kaunti yake kwa kujigamba sana kwenye mitandao ya kijamii
- Waititu kipitia ukurasa wake wa Facebook alisema kuwa afisa huyo alikuwa akitumia wakati wake mwingi kuchapisha picha kwenye mitandao ya kijamii na kusahau kutekeleza wajibu wake
- John Mugwe alipewa likizo ya lazima ya siku 30 ambayo ilizua hisia tofauti miongoni mwa wakazi wa Kiambu
Gavana wa kaunti ya Kiambu, Ferdinand Waititu aliwashangaza wengi baada ya kumpatia likizo ya lazima afisa wake mmoja mtendaji kwa kutumia sana mitandao ya kijamii.
Habari Nyingine: Mambo 10 ambayo kila mwanamke anapaswa kuzingatia kabla ya kuolewa
Waititu alidai kuwa afisa huyo alikuwa akitumia wakati mwingi kujigamba kwenye mitandao ya kijamii badala ya kufanya kazi aliyochaguliwa kufanya.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Afisa huyo aliyetambulika kwa majina kama John Mugwe alipewa likizo ya lazima kwa kuchapisha picha nyingi kwenye ukurasa wake wa Facebook na wa Whatsapp akijivunia kazi yake.
Kulingana na taarifa za Standard, Mugwe alipewa likizo hiyo ya lazima ya siku 30 kutoka Jumamosi Aprili 28.
" Nitakuwa na mkutano na wewe baada ya siku zako za likizo kumalizika na tukubaliane jinsi ya wewe utakavyofanya kazi ili kutimiza wajibu wako kwa wakazi wa Kiambu," Waititu alisema.
Waititu anasemekana kughadhabishwa na afisa huyo kwa kutumia wakati wake mwingi kuchapisha picha kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuwahudumia wakazi wa Kiambu.
" Kama kazi yako ni kupigwa picha na kuweka kwenye Facebook na Whatsapp hatutakubaliana na wewe," Waititu alisema.
Ninaweza sema kwamba nazindua mrandi huu lakini sio wangu, ila ni wa mwakilishi wa wadi wa eneo hili, hivyo basi siwezi ingilia kati na nichapishe picha kwenye mitandao na kuwaarifu watu kwamba nafanya kazi usiku na mchana, heri ukweli usemwe, hakuna haja ya watu kujifanya kuwa wanafanya kazi kwa niaba ya wengine," Gavana Waititu alisema.
Habari Nyingine: Mcheshi Chipukeezy anamtafuta mwanamke aliyepatikana na naibu gavana wa Kirinyaga
Afisa huyo anasemekana kuwa miongoni mwa wanasiasa waliounda chama cha United for Kiambu kilichompigia debe Waititu wakati wa kampeni za mwaka wa 2017.
Akiwa mwenye ghadhabu, afisa huyo alisema kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa anashangazwa ni vipi amesimamishwa kazi kwani amekuwa akifanya kazi yake vipasavyo.
" Mimi John Mugwe nimearifiwa kuenda likizo ya lazima kwa muda wa siku 30 kuanzia leo, jambo hili linashangaza lakini sina la ziada, ninachoamini ni kwamba nitaendelea kuwahudumia wakazi wa Kiambu baada ya likizo yangu," Mugwe aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Habari Nyingine: Gavana Joho asema alikuwa likizo ya miezi miwili
Inasemekana Mugwe alikuwa mstari wa mbele kupinga uongozi wa aliyekuwa gavana wa Kiambu, William Kabogo lakini Waititu amekuwa na uhusiano mbaya naye tangu alipochaguliwa kuwa gavana wa Kiambu Agosti 8.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Tazama habari zaidi kutoka hapa TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibH91fpNmrpqhpJ7BtnnApp2urJFiuKLGyGaumrKZp7Zurc2asJ6olaOxonnKrquupZmWeq6105qlnZmfYsaiecqioZqlmZ57qcDMpQ%3D%3D