Jamaa wawili wauawa Embu kwa kukatwakatwa kwa mapanga baada ya kuiba kuku
- Wanaume wawili walikatwakatwa kwa mapanga na kufariki papo hapo baada ya kupatikana wakiwa wameiba kuku wa jirani wao kijijini Ugweri kaunti ya Embu
- Baada ya kuuawa na wakazi wenye hamaki, miili ya wawili hao iliripotiwa kuchomwa kwa kumwagiwa petroli
Wanaume wawili kutoka kijiji cha Ugweri kaunti ya Embu waliuawa na wakazi wenye hamaki kwa kukatwakatwa kwa mapanga baada ya kupatikana wakiwa wameiba kuku wa jirani
Afisa mkuu wa kituo cha polisi cha Ugweri Peter Muchemi alisema kuwa mfugaji kuku hizo alisikia kelele kutoka nyumba wanamolala kuku wake na alipoenda kuangalia kilichokuwa kikiendelea, aligundua kuwa kuku wawili walikuwa wameibwa.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Aliwaarifu majirani wake waliokuja kwa hasira na kuanza kufanya msako mkali katika kijiji hicho.
Kulingana naibu wa chifu Patrick Irungu washukiwa hao walipatikana wakipika kuku hao mita 300 kutoka pale walipoiba kuku hao.
Wanakijiji waliwashambulia vilivyo kwa kuwakatakata kwa mapanga na baadaye kuchoma miili ya washukiwa hao.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4V1gZRmoZqlkZZ6uK3WoqOiZaeWwqLDwGacppqlYri4rYykrKSZpKyurK3TsJhmo6eWeq6tz5qloJldl66isMBmsJplm6q2o62MpKykrV6dwa64