Aliyekuwa jambazi sugu asimulia alivyoponea kifo kabla ya kuokoka
- Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo amewatia moyo watu wengi kwenye mitandao ya kijamii akitoa ushuhuda wa alivyokuwa jambazi wa benki
- Mvulana huyo aliyejitambulisha kama Japs Kenya aliwasihi wahalifu kubadili mienendo yao
- Japs alitumia mfano wa maisha yake ya ujambazi kujaribu kugeuza mienendo ya vijana waliopotoka
Mvulana mmoja mwenye umri wa makamo aliwaacha Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wakivuja hisia baada yake kufichua jinsi alivyokuwa jambazi wa kuiba benki.
Jamaa huyo kwa jina Japs Kenya siku ya Jumanne, Februari 6, 2018 alifichua kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook jinsi alivyotekeleza wizi kwa kutumia bunduki.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: Kula kwa macho: Dadake Diamond awaonyesha mashabiki chupi yake akiwa jukwaani
Kwenye kipachiko kirefu kilichotazamwa na TUKO.co.ke, Japs alieleza jinsi mjombake ambaye walishirikiana katika ujambazi alivyopigwa risasi na kuuwawa katika mojawapo ya wizi wao kwenye benki uliotibuka.
Habari Nyingine: Mourinho asalimu amri na kuitaja klabu itakayoshinda ligi ya Uingereza
Habari Nyingine: Mwili wangu haujakusudiwa jela - Musalia Mudavadi
“USHUHUDA: Mimi ni jambazi aliyebahatika kuishi, sikuuwawa. Mjombangu aliuwawa kwa kupigwa risasi tulipokuwa tukijaribu kuiba kwenye benki. Tulikuwa na bunduki!!!” Japs aliandika.
Japs alifichua kuwa alikuwa akitafuta bunduki kutoka eneo la Pokot na kuzitumia kwa ujambazi.
Katika ujumbe aliousambaza kwenye kikundi cha Facebook cha Dandora Crime Free, Japs alisema alilazimika kuasi ujambazi alipokamatwa na kukuhukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya wizi wao katika benki kutibuka.
Habari Nyingine: Nikifa mtoto wangu asiguse jeneza langu, babake Diamond afoka
“Wawili kati ya wale tulioshirikiana nao kufanya ujambazi walitoroka. Nilikamatwa na kufungwa gerezani. Bunduki tulizokuwa nazo zilitwaliwa na polisi, bunduki halisi kutoka Pokot, wacha hizi ghushi mnaita dikwara. Nilitumia bunduki halisi. Nilifungwa kwa miaka miwili (2009-2011).” Japs aliongeza.
Baada ya kifungo hicho, Japs aliamua kuwacha ujambazi na kuokoka. Baadaye aliamua kutafuta kazi nzuri ili kukidhi mahitaji ya mkewe na mwanawe.
“Niliamua kumfuata Yesu. Aliniokoa kutoka gizani kutoka mwaka wa 2011 mpaka leo. Nilitafuta kazi ya mhudumu wa hoteli na sasa ninaishi maisha huru. Makarao waliacha kunifuata. Nina dem na tuna mtoi mmoja.” BADILISHA MAISHA YAKO IWE BORA ZAIDI. KAMA UKO HAI, HUJACHELEWA.” Japs aliandika.
Habari Nyingine: Je wanaume wanahitaji nini katika uhusiano? Wakenya watoa maoni yao
Japs aliwataka vijana wenzake kutojiunga na uhalifu na ujambazi, akiwahimiza majambazi kugeuza mienendo yao kwa kuwa hawajachelewa.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una taarifa ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Raila Odinga aapishwa kuwa rais wa wananchi – Kwenye TUKO TV
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4J1g5RmmKWhqZq4tsPAZqGapZKWx6p50q6ermWRqLauwcuimGaZnJ7DurvPqKWemV2gtqe7jKSYm6SRYsaiecqupqSnm5Z7qcDMpQ%3D%3D