Je, huyu ndiye jamaa anayemzingua kipusa wa Diamond kitandani?

Publish date: 2024-07-22

-Hamisa Mobetto ana mpenzi mwingine ikiwa picha yake iliyotazamwa na TUKO.co.ke ina kiashirio

-Hamisa ambaye amemzalia Diamond Platinumz mtoto alipachika picha ya mwanamume mwengine kwenye mitandao ya kijamii na kudokeza uwezekano wa kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi

-Hatua hiyo iliongeza sarakasi katika wingu la mapenzi inayowahusisha Diamond Platinumz na mama ya watoto wake, Zari Hassan

Kipusa wa pembeni wa Diamond Platinumz amepiga hatua ambayo itawaacha Platinumz mdomo wazi

Kipusa huyo ambaye amekuwa akimchumbia Diamond kisiri kwa karibu miaka kumi amezua maswali kwa umma baada ya kupachika picha ya mwanamume mwingine anayeaminika kuwa mpenzi wake mpya.

Jumanne, Novemba 7 2017, Hamisa kwenye Facebook alipachika picha yake akiwa amesimama karibu na jamaa mrefu na mweupe, kipachiko ambacho kiliwaacha wengi wakijiuliza ikiwa jamaa huyo alikuwa mpenzi wake wa kuchukuwa nafasi ya Diamond.

Habari Nyingine: Mke wangu hujibu jumbe zilizotumwa na wanawake kwenye simu yangu – afichua Njugush

Habari Nyingine: Acha kumnyemelea mke wa nduguyo – Mke amkanya mumewe

Picha hiyo ilikuwa nzuri tu, lakini alichoandika Hamisa iliashiria kuwa huenda amechukuwa hatua nyingine ya kuwa na mwamamume mwingine.

“??”Hamisa alipiga picha hiyo

Baada ya muda mfupii, watu walimiminika kwenye ukurasa wa Hamisa kumpongeza kwa kupata kipenzi kipya.

Habari Nyingine: Nisaidieni, Mume wangu ameshindwa kuwacha ‘mipango ya kando’

Hatua ya Hamisa inajiri wakati wingu la mapenzi limemgubika Diamond na mamake wana wa Diamond, Zari Hassan.

Kama iliyoripotiwa na TUKO.co.ke hapo awali, Hamisa na Diamond wamekuwa wakichumbiana kisiri kwa muda sasa na hata wana watoto pamoja.

Habari za uhusiano huo ulisabarisha sarakasi, mama ya wana wengine wa Diamond, Zari Hassan akitishia kumwacha msanii huyo wa bongo.

Habari Nyingine: Kidosho amwaibisha pasta kwa kukosa kulipa deni lake

Diamond amekuwa akijaribu kurejesha uhusiano wa kawaida kati yake na Zari, lakini Zari alionekana kuamua kuendelea na maisha yake pekee yake.

Hata hivyo, TUKO.co.ke haiwezi kuthibitisha kuwa mwanamume aliyezungumziwa ni mpenzi mpya wa Hamisa, lakini kwa kudadisi picha hiyo, maoni na kipachiko cha Hamisa, chochote chaweza kuwa kinaendelea.

Hamisa alimzalia Diamond mtoto mvulana mwezi Agosti 2017 na wamekuwa na ubishi baada ya tukio hilo.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una taarifa ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri:mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaoRzfJRmoZ5lmKrGtnnNnaCynV2frq6twGaYp5mpmrq7tc2grJplm569tr%2FAZq6aZZSerq67zZ1kpKGklrulrc2iZaGsnaE%3D