Matokeo ya KCSE ya wasichana yamtia taabani Waziri Matiangi
- Waziri wa Elimu Fred Matiang’i yuko taabani kwa mara nyingine kuhusu matokeo ya KCSE 2016
- Uchanganuzi wa data za mtihani na zile za jinsia umebaini hitilafu katika matokeo yaliyotolewa; unaashiria kuwa alama za wavulana zilipewa wasichana, nazo za wasichana zikapewa wavulana
Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne (KCSE) 2016 yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu Fred Matiang’i, yaonyesha kuwa wanafunzi wasichana walifanya vyema zaidi kuliko wavulana.
Hata hivyo, uchanganuzi uliofanywa na Nation Newsplex unaashiria kuwa yawezakana alama hizo zilichanganywa.
Habari Nyingine: Waziri Matiang'i asemekana kufanya MAKOSA makubwa kwenye KCSE 2016
Orodha iliyotolewa na matokeo ilionyesha watahiniwa 571,161 walifanya mtihani huo – 299,268 walikuwa wasichana na 271,893 wavulana.
Hata hivyo, takwimu za Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) zaonyesha ni watahiniwa 574,125 walifanya mtihani; wasichana walikuwa 273,130, wavulana walikuwa 300,995.
Pata HAPA habari za TUKO.co.ke punde tu zinapochapishwa!
Hii inamaanisha kuwa idadi wa wavulana ilipingua kwa 29,102 ilhali ya wasichana iliongezeka kwa 26,138 jambo ambalo halikubainika kamwe.
Hivyo, wasichana waliopewa alama walikuwa wengi kuliko waliofanya mtihani, hali ambayo itaibua sintofahamu kuu.
Habari Nyingine: Wasichana wapepea KCSE, wanaume waitisha kikao cha dharura!
Wakati akitangaza matokeo, waziri Matiang’i alieleza kuwa kuna wanafunzi ambao hawakupewa alama yoyote kwa sababu walikosa kufanya mitihani ya masomo isiyopungua 7 kama inavyotakiwa.
Hata hivyo, uchambuzi wa Nation Newsplex waonyesha ufafanuzi wa Matiang’i haujajumuisha idadi hiyo ya wanafunzi isiyokuwepo.
Uchambuzi huu unakujia majuma kadha baada ya Chama cha Walimu (KNUT) kudai kuwa hitilafu chungu nzima zilitia dosari shughuli ya kusahihisha mitihani, na kwamba matokeo hayakuainishwa kama ambavyo imekuwa ikifanyika.
Habari Nyingine: Jamaa wa miaka 43 azungumza baada ya kupata D katika KCSE 2016
KNUT inataka matokeo ya KCSE 2016 yafutiliwe mbali na shughuli ya kuainisha alama za wanafunzi ifanyiwe mitihani hiyo ilia lama ziwe za kuaminika. Ni kauli ambayo Matiang’i ameipuuza kabisa akisisitiza matokeo yalikuwa sahihi na hayatasahihishwa upya.
Tazama Matiang'i akitetea matokeo ya KCSE 2016:
Subscribe to watch new videosRead ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: aron.mtunji@tuko.co.ke
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiZ4R2fJJmpJqsn6CysHnYmmSkm6OaerqtjLCYrKGTna6vrYyymKasmZZ6ta3Am5inoV2srru10aJkppmknq6vs8hnn62lnA%3D%3D